Liwali 'amezwa' na shimo barabarani Texas, Marekani

Mpita njia alisaidia mwenye gari jingine ambalo pia lilikuwa limetumbukia kwenye shimo hilo Haki miliki ya picha AP
Image caption Mpita njia alisaidia mwenye gari jingine ambalo pia lilikuwa limetumbukia kwenye shimo hilo

Liwali ambaye hakuwa kazini alifariki baada ya gari lake kutumbukia kwenye shimo lililojaa maji, ambalo lilizuka ghafla katika eneo la San Antonio, jimbo la Texas nchini Marekani.

Maafisa wanasema Dora Linda Nishihara, 69, ambaye ni naibu liwali aliyekuwa anahudumu kama afisa wa kutekeleza maagizo ya mahakama, alifariki baada ya gari lake kutumbukia kwenye shimo hilo la kina cha futi 12 (3.6m).

Maliwali huchaguliwa na umma Marekani na huwa na majukumu yanayokaribiana na ya maafisa wa polisi.

Gari lake liliondolewa kutoka kwenye shimo hilo kwa kutumia kreni baadaye Jumatatu.

Gari la pili pia lilitumbukia kwenye shimo hilo. Watu wawili waliokuwa kwenye gari hilo waliokolewa na wapita njia wakiwa na majeraha.

Gari la Bi Nishihara lilikuwa limepinduka kabisa na kufunikwa na maji shimoni.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa San Antonio wakilitoa gari la Nishihara shimoni

Maji kwenye shimo hilo yanadaiwa kutoka kwa bomba la maji taka lililokuwa limetoboka.

Liwali wa wilaya ya Bexar Susan Pamerleau amesema idara yake imesikitishwa sana na kisa hicho na anasaidia familia ya marehemu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii