Wazazi ambao hujuta kwa kuzaa watoto

Mama na mtoto Haki miliki ya picha Mary Evans Picture Library
Image caption Mama na mtoto

Mwandishi mmoja kutoka Ufaransa Corinne Maier, ana watoto wawili lakini ndoto yake ni kumuona kitinda mimba akikua na kuondoka nyumbani, akisema kuwa wamemchosha na kumfilisi.

Yafuatayo ni baaadhi ya maoni ya wazazi wengi duniani kuhusu kuwalea watoto.

Majuto

Ni vizuri kufahamu kuwa si mimi peke yangu ninahisi kutokamilika kwa kuwa mama. Nikiwa ninawapenda watoto wangu wawili sana, leo hii ninahisi kuwa singewazaa watoto hawa. Sio tu ni ghalia, lakini kuwalea watoto kunakuja na changamoto nyingi za kukua kitaaluma, wanawake wanalazimika kusubiri hadi zaidi ya miaka 35. Kuna sababu za kuhusu raha ya kuwa mama, lakini nahisi kuchoka na kutokamilika. Alex, San Antonio.

Ni vigumu kusema kuwa ninajutia kwa kuwa na watoto kwa sababu ninawapenda. Lakini ikiwa nitafikiria nyuma na kujiuliza maswalia, sidhani kama ningetaka tena kuwa na watoto, bila ya wao ningekuwa na pesa, uhuru na pia singekuwa na hofu. Mary, Edinburgh.

Haki miliki ya picha iStock
Image caption Mama na mtoto

Baada ya kulelewa katika familia iliyovunjika, nimekuwa na ndoto ya kuwa na familia kubwa. Nimebarikiwa na mme mzuri na watoto watatu. Wakati nikiandika haya binti yangu amenishika shingoni , siwezi hata kwenda chooni bila kukosa kusikia kilio na vita na jina mama. Krismasi imewadia na badala ya kufurahia, ninahisi kama ningeingia kwa ndege na mmewangu na kwenda popote pasipo kurudi ili kuweza kumjua tena. Tumechoka sana hadi hata siku hizi hatucheki, vile ninaandika haya ninahisi vibaya lakini ninahitaji nishukuru. Andrea, Italy.

Haki miliki ya picha iStock
Image caption Wazazi waliochoka

Kumlea mtoto wa kisasa imetuacha mimi na mme wangu na uchovu. Haishii utotoni kwa sababu tunawahofia wakiwa na miaka 24 na 26 mtawalia. Tulijaribu kuwawezesha wajitegemee lakini tukashindwa. Wanaishi mbali nasi lakini mwishowe ni lazima tuwapigie simu kila mara. Ninawapenda wote lakini kama ningerudi ujana singekuwa tena na watoto. Jennifer,Hertfordshire.

Hisia zilizochanganyika

Nina watoto wawili wa kiume na ninawapenda sana hadi uchovu unapoingia na kelele za kila siku zikionekana kuisha. Nilikuwa mvumilivu na kiali yangu ilikuwa kamili . Hilo linaokena kutoweka. Kwa sasa ni mipango, kulala , chakula, mavazi, kucheza , malezi bora. wakati hali ni ngumu nahisi singekuwa na watoto. Lakini wakati wanakubusu au wanapofanya kitu kizuri kwako unahisi vizuri. Anja, Maastricht.

Hakuna majuto

Kuwa na watoto ndicho kitu kizuri zaidi kuwai kufanyika kwangu. Pia ni kazi ngumu. Sijui mtu anaweza kupata wapi maoni kuwa mzazi ndiyo kazi rahisi ambayo huleta furaha. Kuwa na furaha kwa misingi yote ni kitu ambacho mtu hukutafuta kwa muda mrefu. Brian, Ohio.

Sitafikiria tena kutokuwa na watoto. Wameniwezesha kujua mengi kupitia kwa walimu wao, na wazazi wengine.Karen, Virginia.

Haki miliki ya picha iStock
Image caption Baba na mtoto wakicheza

Kuwa na mtoto kumeniwezesha kuenzi masuala mengi ya kijamii. Niliandika kitabu kwa mtoto wangu wa kiume, ambacho nilimtumia ajenti mmoja na miaka michache baadaye, nimejipata nikiwa mwandishi wa vitabu vya watoto nikiwa na vitabu kadha ambavyo nimeviandika.. Ninaelewa kuwa singeyafanya hayo kama singekuwa na huyu mtoto. Tumensafiri sana, alisaidia kukutana na watotu wengi. Sam, Worthing.

Niliwalea watoto wawili nchini Japan. Ndiyo ilinigharimu sana kifedha na muda, lakini nimeweza kufanikiwa kitaalumaa. Watoto waliniwezesha kuwa na mipango nadhifu. Kwa ujumla watoto wamerejesha mengi sawa na yale walipewa Bob, Tokyo.

Mada zinazohusiana