Raia wajitokeza kwa wingi kupiga kura Ghana

Raia wajitokeza kwa wingi kupiga kura Ghana

Raia nchini Ghana leo wanapiga kura kuchagua rais mpya na wabunge katika uchaguzi ambao wachambuzi wanasema huenda ukawa na ushindani mkubwa.

Uchumi mbaya na rushwa ndio yamekuwa tatizo kuu nchini.

Kumeshuhudia visa kadha vya ghasia za kisiasa katika kuelekea uchaguzi huu.

Ushindani mkali ni kati ya Rais John Mahama na kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Nana Akufo Addo.