Ajali iliyomuua katibu mkuu wa UN Dag Hammarskjold kuchunguzwa

Dag Hammarskjold Haki miliki ya picha AP
Image caption Dag Hammarskjold

Azimio linawasilishwa kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, likitaka kufanyika uchunguzi kuhusu ajali ya ndege iliyotokea mwaka 1961, ambayo ilisababasha kifo cha aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo, Dag Hammarskjold.

Ndege hiyo ilianguka eneo ambalo iko sasa nchi ya Zambia, wakati wa ziara ya kidiplomasia kujaribu kuleta usitishwaji wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo.

Wakati huo makosa ya rubani yalitajwa kuwa sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo.

Hata hivyo ushahidi mpya umeibuka ambao huenda ukaongeza shaka kuwa ajali hiyo ilipangwa.

Azimio hilo linazilazimisha nchi kusalamisha nyaraka na sauti za mawasiliano ya radio kwa mchunguzi maalum ambazo huenda zikafichua ukweli kuhusu kile haswa kilifanyika

Bwana Hammarskjold na wasaidizi wake walikuwa wakielekea eneo la Ndola ambalo sasa liko nchini Zambia, kukutana na Moise Tshombe ambaye alikuwa ametangaza uhuru wa eneo lenye utajiri wa madini la katanga.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndege hiyo ilianguka gizani kwenye msitu karibu na Ndola muda mfupi kabla ya kutu

Ndege hiyo ilianguka gizani kwenye msitu karibu na Ndola muda mfupi kabla ya kutua na kumuua raia huo wa Sweden na watu wengi 15 waliokuwa nadani .

Chanzo cha ajali hakijaelezwa kwa njia kamali licha ya kufanyika uchunguzi mara tatu.

Uchunguzi wa tatu uliofanywa na Umoja wa Mataifa mwaka 1962 haukukana kuwepo shambulizi

Kisha mwaka 2015 Umoja wa Mataofa ulibuni jopo la wataalamu kutathmini ushahidi mpya katika kesi hiyo

Mwandishi wa BBC anasema kuwa taarifa za hivi majuzi zaidi zinataja kuwepe kwa wanaume wazungu waliokuwa kwenye gari nyeupe katribu na eneo ajalia ilitokea.