Ndege yaanguka ikiwa na abiria 48 Pakistan

Mabaki ya ndege yakiteketea eneo la ajali Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mabaki ya ndege yakiteketea eneo la ajali

Ndege mmoja ya shirika la ndege Pakistan (PIA) iliyokuwa imewabeba abiria 48 imeanguka kaskazini mwa nchi hiyo.

Ndege hiyo aina ya PK-661, ilipoteza mawasiliano na mnara wa waelekezi wa ndege ilipokuwa ikitoka Chitral ikielekea Islamabad muda mfupi baada ya kupaa angani,'' shirika hilo limesema katika taarifa yake.

Ndege hiyo ya taifa imelaumiwa kwa kukosa kuimarisha usalama kwa siku za hivi karibuni.

Ajali kubwa ilitokea mwaka 2006 iliowaua watu 44.

Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Havelian, karibu kilomita 70 (maili 43) kaskazini mwa Islamabad kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege sawa na yenye ilianguka ikijiandaa kuruka mwaka 2015

Ndege hiyo ilipaa kutoka Chitral saa 10:00 GMT, na kupoteza mawasiliano dakika 90 baadaye, muda mfupi kabla ya kufika Islamabad, vyombo vya habari vimeripoti.

Nyota wa zamani wa nyimbo ya pop aliyebadilika kuwa muhubiri wa kislamu , Junaid Jamshed na mkewe walikuwa miongoni mwa abiria kwenye ndege hiyo, kulingana na kituo kibinafsi cha televisheni cha habari cha GEO.

Jeshi limesema limewatuma wanajeshi na ndege za helikopta kwenye tukio la mkasa,

Umoja wa mataifa ilipiga marufuku ndege za shirika hilo la PIA kuelekea barani Ulaya mwaka 2007 kutokana na hali yao ya kiusalama.