Bibi awa mama Uingereza

Uingereza
Image caption Julie Bradford alibeba ujauzito kwa niaba ya bintiye Jesica

Ama kweli ,duniani kuna mambo!Mwanamke mmoja ameamua kubeba mimba, kuzaa mtoto kwa niaba ya bintiye.Mwanamke huyo jina lake ni Julie Bradford, mwenye umri wa miaka 45, alijifungua mtoto aitwaye Jack kwa niaba ya bintiye Jessica Jenkins, ambaye yuko katika matibabu ya ugonjwa wa saratani ambao umesababisha awe tasa.

Jessica, mwenye umri wa miaka 21, mwenyeji wa Rhymney, aliamua kupeleka mayai yake kugandishwa katika chuo kikuu cha utabibu cha Cardiff huko Wales kabla hajaanza matibabu yake ya saratani ya kizazi yalianza miaka mitatu iliyopita.

Jesica anasema tangu akiwa binti mdogo alikuwa na ndoto ya kuwa mama, na sasa ndoto yake imetimia, Jesica na mumewe Rees waliamua kutumia njia ya uzazi ya kupandikiza mapema mwaka huu.

Jesica aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani mnamo mwaka 2013, alipokuwa na umri wa miaka 18 wakati ambao madaktari waliona ni mapema mno kumuanzishia matibabu ya kansa ya kizazi .

Jesica anatoa ushuhuda kwamba madaktari walifanikiwa kuchukua mayai ishirini na moja tumboni mwake kabla ya kuanza matibabu na kati ya hayo ni mayai 10 ndiyo yaliyo nusurika yakaoteshwa kwa wiki mbili na baadaye kugandishwa, na mwezi wa tano mwaka huu yaliyeyushwa na kuwekwa tumboni mwa mamake Jesica na hivyo kumpa nafasi ya kuishi mtoto Jack na kukua tumboni mwa bibi yake.

Mamake Jesica anasema kwamba bintiye alipopewa taarifa za ugonjwa wake alijiona hana thamani tena na ndoto yake ya kuwa mama kuzimwa na saratani ya kizazi, wakati saratani ilipoondoa uwezekano wa Jess kubeba ujauzito wote tulikufa moyo.

Nikaamua kuwa nitabeba ujauzito kwa niaba yake na itakuwa fahari kuwabebea ujauzito kwa heshima ya familia ya mwanangu, tumetumia muda mwingi katika hospitali mbali mbali limekuwa jambo la kawaida kwetu. Nina furaha ya ajabu kwamba mara hii imekuwa kwa sababu maalum.