Wafanyakazi wa umma watishia kugoma Kenya

Wafanyakazi wa umma watisha kugoma Kenya
Image caption Wafanyakazi wa umma watisha kugoma Kenya

Chama cha wafanyakazi wa serikali kimeonya kuwa kitatangaza mgomo ikiwa serikali haitatatua mzozo kati yake na madaktari chini ya saa 24.

Mgomo wa madaktari ambao uko siku yake ya nne, umeathiri huduma kwenye hospitali za umma huku wafanyakazi wa sekta ya umma wakidai kuwa lazima iheshimu kutekelezwa kwa mkataba uliotiwa sahahi mwaka 2013.

Chama cha madaktari kinasema kuwa kimejiondoa kutoka kwa mazungumzo yoyote na serikali na watarudi tu mezani kujadili njia ya kutekelezwa kwa makubaliano yao.