Nyimbo za Tanzania zilipendwa zaidi Kenya 2016

Image caption Diamond Platinumz alipokuwa anahojiwa BBC 1Xtra

Video za muziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania ndizo zilizotazamwa zaidi na Wakenya katika mtandao wa YouTube, unaomilikiwa na Google, mwaka huu, takwimu zinaonyesha.

Video hizo zinatawala katika orodha ya video kumi zilizotazamwa zaidi, inayoongoza ikiwa video ya wimbo Salome, uliofanywa upya na Diamond Platnumz na Rayvanny.

Wimbo wa Work, wao Rihanna na Drake ni wa pili lakini kutoka hapo anaingia Diamond Platnumz na Harmonize wakiwa na wimbo wao Bado.

Video ya kwanza ya Wakenya kwenye orodha hiyo ni ya Sauti Sol kwa wimbo wao Unconditionally Bae, lakini bado kwenye wimbo huo walishirikiana na mwanamuziki Mtanzania, Alikiba.

Video nyingine za nyimbo katika orodha hiyo ni Work from Home wa Mmarekani Ty Dolla Sign na kundi la wasichana la Fifth Harmony, This is What You Came For wake raia wa Scotland Calvin Harris, Kwetu wake Rayvanny kutoka Tanzania, Cheap Thrills wao raia wa Australia Sia na Sean Paul wa Jamaica, Pillow Talk wa Mwingereza Zayn na Ain't Your Mama wa Mmarekani Jenniffer Lopez.

Orodha kamili:

  1. Salome - Diamond Platnumz na Rayvanny.
  2. Work - Rihanna na Drake
  3. Bado - Diamond Platnumz na Harmonize
  4. Sauti Sol - Unconditionally Bae, na Alikiba.
  5. Work from Home - Ty Dolla Sign na Fifth Harmony
  6. This is What You Came For - Calvin Harris
  7. Kwetu - Rayvanny
  8. Cheap Thrills - Sia na Sean Paul
  9. Pillow Talk - Zayn
  10. Ain't Your Mama - Jenniffer Lopez.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii