BBC yasaidia kuongeza wanawake Wikipedia

BBC yasaidia kuongeza wanawake Wikipedia

Huenda hukugundua kuwa taarifa za wanawake maarufu walio katika Wikipedia ni chini ya asilimia 20 pekee. Lakini hilo huenda likabadilika, tushukuru sana harakati za sehemu ya mfululizo wa makala za Wanawake 100 hapa BBC.

Taarifa za wanawake maarufu Alhamisi ziliandikwa kutoka maeneo mbalimbali duniani, hasa waliosahauliwa. Wengi wakiwa waasisi wa sayansi, wanasiasa au wasanii.

Miongoni mwa wanawake na mabinti waliofika afisi za BBC London na kuandika maelezo ya wanawake maarufu Wikipedia ni Blandina Andrew.