Mahama: Nitaheshimu matokeo ya uchaguzi Ghana

Huwezi kusikiliza tena
Mahama na Akufo-Addo: Nani mshindi wa urais Ghana?

Rais wa Ghana John Mahama amesema kuwa ataheshimu matokeo ya uchaguzi wa urais kwenye kinyang'nyiro kikali.

Pia kupitia kwa akaunti yake ya Twitter Mahama alisema kuwa tume ya uchaguzi ni lazima ipewe muda wa kutekeleza wajibu wake.

Vyombo vya habari nchini Ghaba vinasema kuwa mgombea wa upinzani Nana Addo Dankwa Akufo-Addo, mwenye umri wa miaka 72 anongoza.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kabla ya Jumamosi.

Haki miliki ya picha AFP/getty
Image caption John Mahama (kushoto) na Akufo-Addo (kulia)

Tume ya uchaguzi ilitangaza Alhamisi kuwa ilikuwa ikikagua kura hizo kwa njia ya kawaida kwa sababu mfumo wake wa kielektroniki ulikuwa umevurugwa na wadukuzi wa mitandao.

Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika baadaye mwezi huu ikiwa hakuna mgombea kati ya wagombea wakuu hatapata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Kameni ya uchaguzi ilitawaliwa na uchumi unaporomoka.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2012, bwana Mahama alishindwa na bwana Akufo-Addo na chini ya kura 300,000.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii