Mahama na Akufo-Addo: Nani mshindi wa urais Ghana?

Mahama na Akufo-Addo: Nani mshindi wa urais Ghana?

Tume ya taifa ya uchaguzi Ghana bado haijatangaza matokeo, lakini kumeanza kutokea wasiwasi kwenye kambi za vyama vikuu viwili vya siasa nchini humo.

Wafuasi wa chama tawala cha NDC na chama cha upinzani NPP wamekuwa wakisherehekea katika makao ya viongozi wao mjini Accra, kila mmoja akiamini kwamba ataibuka mshindi.

Mwandishi wa BBC Salim Kikeke amefika maeneo hayo na kuandaa taarifa hii.