Polisi wavalia viatu vya kike Uganda kutetea wanawake

Maafisa wa polisi Haki miliki ya picha @PoliceUg

Maafisa kadha wa polisi wa kiume nchini Uganda leo walivalia viatu vya kike na kushiriki katika matembezi kwa lengo la kuhamasisha jamii dhidi ya udhalilishaji na dhuluma dhidi ya wanawake.

Polisi hao walikuwa wanashiriki katika matembezi yafahamikayo kama 'Walk A Mile in Her Shoes' (Tembea Maili Moja na Kiatu Chake).

Picha za maafisa waliovalia viatu hivyo zimesambazwa sana mtandaoni.

Polisi hao waliandaa matembezi hayo kwa ushirikiano na mashirika ya kutetea haki za wanawake.

Shirika la Walk A Mile in Her Shoes linaloandaa matembezi hayo lilianzishwa mwaka 2001 na Frank Baird. Lilianza kama kundi la wanawake waliokuwa wakijitokeza na kutembea kwenye bustani wakiwa wamevalia viatu vya wanawake.

Lakini sasa limekuwa shirika kubwa na kila mwaka maelfu ya watu hushiriki kuchangisha pesa za kusaidia vituo vinavyowasaidia waathiriwa wa ubakaji, waathiriwa wa dhuluma nyumbani pamoja na miradi inayokabiliana au kupinga dhuluma na unyanyasaji wa wanawake.

Haki miliki ya picha @PoliceUg
Haki miliki ya picha @PoliceUg