Kashfa ya ufisadi yakumba afisi ya rais wa Brazil

Rais Michel Temer wa Brazil akumbwa na kashfa ya ufisadi
Image caption Rais Michel Temer wa Brazil akumbwa na kashfa ya ufisadi

Afisi ya rais wa Brazil imekanusha madai kuwa chama cha Michel Temer kilipokea mchango haramu kutoka kwa kampuni ya ujenzi.

Hiyo ni kashfa mpya zaidi kuwahi kukumba chama cha rais Temer cha PMDB tangu atwae madaraka kutoka kwa Dilma Rousseff, Agosti mwaka huu.

Afisa mkuu kutoka kampuni ya Odebretch amewambia maafisa wa mashtaka katika uchunguzi wa awali kuwa alihudhuria kikao cha chakula cha jioni mwaka 2014, ambako alimwomba kiongozi wa kampuni hiyo dola milioni tatu zitumiwe kwa kampeni.

Inadaiwa kuwa Bw Temer aliahidi kutumia mamlaka yake katika bunge la Congress kuiunga mkono kampuni hiyo ya ujenzi.

Afisi ya rais ilisema michango yote iliyotolewa na kampuni ya Ode-brectch ilitangazwa hadharani.