CIA: Urusi ''ilimsaidia Trump kushinda uchaguzi''

Vitengo vya ujasusi nchini Marekani vinasema kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchainda uchaguzi wa Marekani
Image caption Vitengo vya ujasusi nchini Marekani vinasema kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchainda uchaguzi wa Marekani

Vitengo vya ujasusi nchini Marekani vinaamini kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani ili kumpiga jeki Donald Trump katika uchaguzi huo kulingana na maafisa wa Marekani.

Ripoti moja katika gazeti la New York Times inasema kuwa vitengo hivyo vina uhakika wa kiwango cha juu kuhusu hatua hiyo ya Urusi ya udukuzi.

Ripoti nyengine ya maafisa hao iliotolewa na Gazeti la Washington Post pia ilitoa maoni kama hayo.

Lakini upande wa Bw Trump umepuuzilia mbali matokeo ya ripoti hiyo, ukisema hawa ni watu wale wale waliosema kuwa Sadaam Hussein anamiliki silaha za kuangamiza.

Maafisa wa Urusi kwa mra nyengine wamekana kuhusika na udukuzi wowote wa kumsaidia Trump katika uchaguzi huo.

Siku ya Alhamisi rais Obama alitaka uchunguzi kufanywa kufuatia misururu ya udukuzi wa mitandao inayodaiwa kutekelezwa na Urusi wakati wa uchaguzi.

Udukuzi huo ulilenga barua pepe za chama cha Democratic na mshauri wa mgombea wa urais Hillary Clinton.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii