Talaka kati ya Khloe Kardashian na Lamar Odom yakamilika

Khloe Kardashian na Lamar Odom yakamilika
Image caption Khloe Kardashian na Lamar Odom yakamilika

Talaka kati ya Khloe Kardashian's na mchezaji nyota wa mpira wa vikapu Lamar Odom imekamilika miaka mitatau baada ya nyota huyo wa kipindi cha runinga kuanzisha mpango huo.

Kloe mwenye umri wa miaka 32 alianzisha talaka hiyo mnamo mwezi Disemba 2013 baada ya wawii hao kuwa katika ndoa kwa miaka minne.

Lakini aliisimamisha talaka hiyo baada ya Lamar Odim kupatikana katika mkahawa mmoja akiwa hana fahamu mwaka uliopita.

Image caption Khloe Kardashian, Lamar Odom yakamilika na familia ya Khadashians

Khloe alisema kuwa hali yake ya kiafya ndio sababu moja ya kusitisha talaka hiyo.

Lakini aliendeleza talaka hiyo mnamo mwezi Mei akisema kuwa wameshindwa kuelewana katika ndoa hiyo.