Paolo Gentiloni, ateuliwa waziri mkuu wa Italia

Paolo Gentiloni Haki miliki ya picha AFP
Image caption Paolo Gentiloni

Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Italia Paolo Gentiloni, ameombwa kuunda serikali.

Msemaji wa Rais Sergio Mattarella, alisema kwa bwana Gentiloni, ametajwa kuwa waziri mkuu mpya.

Bwana Gentiloni, mwenye umri wa miaka 62, amesema anaelewa kuwa serikali inahitaji kuundwa haraka, ili kuwatuliza raia wa Italia na washirika.

Vyama vya upinzani vimekana uwezekanowa kuunaga dserikaia ya Umoja.

Jumapili iliyopita raia wa Italia walipiga kura kwa asilimia 59 dhidi ya 41 waliopinga mpango ya bwana Renzi wa kuifanyia mabadiliko katiba.