Mikhail Gorbachev na kumalizika kwa vita baridi

Mikhail Gorbachev akizungumza na BBC, Desemba 2016
Image caption Mikhail Gorbachev, 85, mara nyingi hakubali kufanya mahojiano

Kiongozi wa mwisho wa uliokuwa Muungano wa Usovieti Mikhail Gorbachev, amezishutumu nchi za magharibi kwa kuichokoza Urusi na kupanga njama ya kumuondoa madarakani rais Vladimir Putin .

Wakati wa mahojiano na BBC, kuadhimisha miaka 25 tangu Muungano wa Usovieti uvunjike, Bw Gorbachez alisema anaamini kuwa vyombo vya habari vya nchi za magharibi vimepewa maagizo maalum ya kumchafulia jina bwana Putin na kumfanya aondoke madarakani.

Gorbachev amesema kuwa viongozi wa nchi zilizokuwa kwenye Muungano wa Usovieti zilizojitenga na Urusi mwaka 1991, zilifanya uhalifu na mapindzui, Lakini akaongeza kuwa aliondoka madarakani ili kuzuia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bwana Gorbachez analaumiwa sana na watu nchini Urusi kwa kuvunjwa kwa uliokuwa Muungano wa Usovieti lakini pia anaoneka kama shujaa aliyesaidia kumaliza vita baridi.

Tarehe 21 Desemba mwaka 1991 wakati wa matangazo ya jioni, matangazo yalianza kwa kusema kuwa USSR haipo tena.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tarehe 25 Desemba 1991 Mikhail Gorbachev alijiuzulu na kusababisha kuvunjika kwa USSR

Siku chache baadaye viongozi wa Urusi, Belorussia na Ukrain walikutana kuvunja Muungano wa Usovieti na kubuni mataifa huru.

Gorbachez aidha anawakosoa washirika wa karibu wa Rais Putin akiwemo Igor Sechin, ambaye ni mkuu wa kampuni ya mafuta ya Rosnef, na kumtaja kuwa anayejaribua kushawishi masuala ya nchi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwaka 1987, Bw Gorbachev na aliyekuwa rais Marekani wakitia sahihi mkataba wa nyuklia

Ulikuwa ni uhusiano mzuri kati ya Mikhial Gorbachez na rais wa Marekani Ronald Regan uliochangia kumalizika kwa vita baridi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii