Mfalme wa Rwenzururu afunguliwa mashtaka ya Ugaidi

Charles Wesley Mumbere alifikishwa mahakamani katika mji wa Jinja. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Charles Wesley Mumbere alifikishwa mahakamani katika mji wa Jinja.

Mfalme mmoja nchini Uganda amefunguliwa mashtaka ya ugaidi, wizi na kutaka kuua.

Mashtaka hayo ni tofauti na aliyofunguliwa awalia ya kumuua afisa wa polisi.

Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere alifikishwa mahakamani hii leo katika mji ulio mashariki mwa Uganda wa Jinja.

Mahakama ilifurika na wafuasi wa mfalme pamoja na wabunge kutoka nyumbani kwake.

Alikamatwa tarehe 27 mwezi Novemba kufuati uvamizi uliofanywa na polisi na jeshi katika makao ya kifalme mjini Kasese, magharibi mwa Uganda.

Mapigano kati ya walinzi wa mfalme wa kabila la Bakonzo na jeshi yalisababisha vifo vya watu 80 na wegine zaidi ya 100 wakiwa kwenye kizuizi cha polisi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nyumba nyingi katika ufalme huo zilichomwa moto

Serikali inaulaumu ufalme huo kwa kuwapa mafunzo wanamgambo, kwa lengi la kujitenga kutoka Uganda na kuunda taifa la Yiira, madai ambayo ufalme huo inayakana.

Mfalme huyo amerudishwa rumande katika gereza la Luzira mjini Kampala hadi tarehe 28 mwezi Disemba.