Jeshi ladhibiti jengo la tume ya uchaguzi Gambia

Yahya Jammeh anataka uchaguzi mpya kufanyika

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Yahya Jammeh anataka uchaguzi mpya kufanyika

Vikosi vya usalama nchini Gambia vimechukua udhibiti wa jengo la tume huru ya uchaguzi nchini humo na kuwazuia wafanyakazi kuingia jengo hilo.

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia Alieu Momar Njai, aliiambia BBC kuwa vikosi vilionekana kufuata maagizo wakati vilimzuia kuondoka kwenye majengo ya tume mapema leo.

"Niliondoka. Nikarudi Nyumbani," Njai alisema.

Njai alikaribisha kuwasili kwa viongozi wa nchi magharibi mwa Afrika akisema, "ninatumai kumuomba kuwa Jammeh akubali ushauri na aondoke ofisini."

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Alieu Momar Njai anasema amezuiwa kuingia majengo ya tume

Jeshi linachukua hatua hiyo wakati viongozi kadha wa nchi za magharibu mwa Afrika wakimeo Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia Muhammadu Buhari wa Nigeria na rais wa Ghana John Mahama wakiwa tayari wamewasili nchini Gambia.

Viongozi hao wana nia ya kumshawishi Rais Jammeh kuheshimu matakwa ya watu na kuondoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu.