Mwanamke ajifungua kwa kutumia tishu za ovari za utotoni

Moaza asema atafurahi kuona wanawake wengi wasio na uwezo wa kuzaa wakisaidiwa kupata watoto kwa njia hiyo
Image caption Moaza asema atafurahi kuona wanawake wengi wasio na uwezo wa kuzaa wakisaidiwa kupata watoto kwa njia hiyo

Mwanamke aliyepata mtoto London kwa kutumia tishu za ovari zilizogandiswa akiwa mtoto ameelezea kuzaliwa kwa mtoto wake kama muujiza.

Inasemekana kuwa hii ni mara ya kwanza kwa madaktari popote ulimwenguni kutumia utaalam kama huo kuweza kupata mtoto.

Madaktari wake wanasema kuwa mafanikio hayo yatatoa matumaini zaidi kwa watoto wengine wenye tishu za ovari zilizohifadhiwa kabla ya kufanyiwa matibabu ya saratani.

Image caption Mtoto wa Moaza alizaliwa katika hospitali ya London

Moaza Al Matrooshi,mwenye asili ya Dubai, alizaliwa na matatizo ya mfumo kwenye damu yaliyomfanya asiweze kuzaa akiwa mtu mzima ambapo tishu za ovari zake zilichukuliwa na kuhifadhiwa na wataalam hao wa afya ili kuchanganya na mayai yake atakapokuwa mkubwa kisha kupatikana kwa mtoto.

Image caption Tishu za ovari za Moaza zilivyochukuliwa na kuhifadhiwa