Rais Salva Kiir aitisha mazungumzo ya kitaifa

Rais Kiir amekana taarifa za jeshi lake kuhusika na matendo ya kihalifu
Maelezo ya picha,

Rais Kiir amekana taarifa za jeshi lake kuhusika na matendo ya kihalifu

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ameitisha mazungumzo ya kitaifa yatakayomaliza vita vya vya miaka mitatu vya wenyewe kwa wenyewe.

Akihutubia bunge mjini Juba, amesema jopo la wataalam litaongoza mazungumzo hayo.

Hata hivyo, hakumtaja hasimu wake, ambae alikuwa makamu wa Rais, Riek Machar, ambae alikimbia baada ya mapigano kuzuka mnamo mwezi July.

Afisa wa umoja wa mataifa anaeshughulikia masuala ya haki za bindamu nchini Sudan Kusini ametahadharisha kuzuka upya kwa mapigano ambayo yatahatarisha usalama wa eneo zima.

Rais Kiir amekana taarifa za mara kwa mara zinazotuhumu vikosi vyake kuhusika na mauaji ya halaiki na ubakaji.