Malaika na miungu ni wa rangi gani?
Malaika na miungu ni wa rangi gani?
Mtengenezaji filamu raia wa Kenya Jim Chuchu ameandaa maonesho ya kipekee aliyoyapa jina The Bones Remember (Mifupa Kumbuka).
Anawataka Waafrika kutafakari zaidi kuhusu dini, na kubaini nafasi yao ni gani hasa baada ya kuachana na dini na tamaduni zao za awali.
Anataka kazi yake kuwahamasisha Waafrika kujiuliza: Je, sisi tuko wapi katika imani? Na je, miungu wetu wana rangi gani?