Amnesty: Ethiopia huzima mitandao kudhibiti wapinzani

Amnesty: Ethiopia huzima mitandao kudhibiti wapinzani

Serikali ya Ethiopia imeshutumiwa kwa kufunga tovuti ili kudhibiti mienendo ya matumizi ya mitandao ya kijamii.

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International linasema limepata ushahidi kuwa mitandao maarufu ya kijamii na progamu tumishi kama Facebook au What's App ilifungwa kwa wiki kadhaa wakati wa maandamano ya kupinga serikali.

Mamlaka nchini Ethiopia zinasema wanataka kuwazuia mabloga wasichochee ghasia na fujo.

Intaneti sasa imejerea lakini baadhi ya huduma bado haziwezekani kwani kasi ni ndogo sana.

Mwandishi wetu Emmanuel Igunza anaarifu zaidi kutoka Addis Ababa.