Bunge la Israel laondoa sheria ya sketi fupi

Wafanyakazi kadha walikusanyika mbele ya bunge

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wafanyakazi kadha walikusanyika mbele ya bunge

Bunge la Israeli limetupilia mbali sheria za kuvaa kwa wafanyakazi wa bunge baada ya wafanyakazi hao kupinga sheria zinazowataka kutovalia sketi fupi.

Wafanyajazi hao walidai kuwa walinzi katika bunge walikuwa wakitekeleza sheria hizo na kuwazuia watu kuingia bunge hilo.

Spika Yuli Edelstein alisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa baada ya malalamiko kuhusu mavazi yasiyoridhisha.

Sasa timu itateuliwa kuangalia vile sheria hizo zitatatekelezwa.

Mwezi Oktoba usimamizi wa bunge ulituma barua kuwakumbusha wafanyakazi wote wa bunge kuhusu sheria hiyo ya mavazi.

Sheria hiyo inapiga marufuku fulana, kabtula,pati pati na nguo fupi au sketi lakini haielezi utefu unaotakikana.

Wakati wa maandamano hayo ya siku ya Jumatano watu walivalia sketi fupi kama njia ya kupinga sheria hizo.

Baadhi walisema kwa walilazimishwa kufungua makoti yao na walinzi wa kiume ili wapate kuona urefu ya sketi zao.

Sheria hizo hazijatoa kipimo cha urefu wa sketi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Sheria hizo hazijatoa kipimo cha urefu wa sketi