China yakamata chombo cha Marekani baharini

Chombo cha USNS Bowditch kilikuwa kikifanya utafiti Haki miliki ya picha US Navy
Image caption Chombo cha USNS Bowditch kilikuwa kikifanya utafiti

Marekani imetoa ombi kwa China ikiitaka iwachilie chombo cha baharini ilichokamata katika maeneo ya bahari ya kimataifa.

Jeshi la wanamaji wa China lilikamata chombo hicho cha utafiti wa chini ya bahari, kusini mwa bahari ya China siku ya Alhamis.

Kisa hicho kilitokea wakati meli moja ya Marekani ilikaribia kukiondoa chombo hicho baharini

Chombo hicho kwa jina "naval glider" kinatumiwa kufanyia utafiti viwango vya chumvi baharini na pia vya joto.

"Chombo hicho kilikuwa kikiendesha utafiti kulinga na sheria za kimataifa kusini mwa bahari ya China,"maafisa wa Marekani walisema.