Wanajeshi 13 wauawa kwenye shambulizi Uturuki

Shambulizi hilo ni la bomu la kutegwa ndani ya gari Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulizi hilo ni la bomu la kutegwa ndani ya gari

Shambulizi moja la bomu nchini Uturuki limewaua wanajeshi 13 waliokuwa ndani ya basi na kuwajeruhi wengine 48.

Mlipuko huo uliharibu basi hilo ambalo lilikuwa na wanajeshi waliokuwa wameruhusiwa kusafiri kwenda soko moja, mwa mujibu wa msemaji wa jeshi.

Picha kutoka eneo ambapo mlipuko huo ulitokea zilionysha basi hio likiwa limeharibiwa kabisa na shimo kubwa likionekana upande mmoja.

Mlipuko huo unatokea wiki moja baada watu 44 kuuawa na shambulizi la bomu mjini Istanbul, lililodaiwa kufanywa na wanamgambo wa kurdi.

Uturuki imekumbwa na misurusu ya mashambulizi mabaya mwaka huu wa 2016 mikononi mwa wanamgambo wa kurdi.

Baibu waziri mkuu Veysi Kaynak alisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa sawa na lililoendeshwa na wanamgambo mjini Istanbul.

Serikali imeweka marufuku ya muda ya kutotangazwa kwa shambulizi hilo.

Seriklia imewka mmarufuku a uda ya kutangazwa kjwa shmbualia hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Basi lililoshambuliwa likiwaka moto