Basi lagonga nyumba Uingereza

Basi lagonga nyumba huko Uingereza
Image caption Basi lagonga nyumba huko Uingereza

Takriban watu watano wamejeruhiwa baada ya basi kugonga nyumba moja.

Basi hilo liligonga nyumba hiyo iliopo huko Homer Green karibu na mji wa Wycombe nchini Uingereza.

Abiria watatu walijeruhiwa huku mwanamume na mwanamke waliokuwa ndani ya nyumba hiyo pia wakijeruhiwa.