Rais wa zamani wa Israel Moshe Katsav kuachiliwa huru

Moshe Katsav ndiye rais wa kwanza wa zamani wa Israel kufungwa jela Haki miliki ya picha AFP
Image caption Moshe Katsav ndiye rais wa kwanza wa zamani wa Israel kufungwa jela

Rais wa zamani wa Moshe Katsav anatarajiwa kuachiliwa huru baada ya kukaa miaka mitano jela kwa kosa la ubakaji.

Bodi ya kutoa msamaha kwa wafungwa nchini Israel iliamua Jumapili kwamba Katsav, 71, anaweza kuachiliwa huru wiki ijayo baada yake kukaa miaka mitano jela.

Alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Maombi yake mawili awali ya kutaka kuachiliwa huru mapema yalikuwa yamekataliwa.

Katsav alijizulu wadhifa wa urais mwaka 2007 baada ya kufunguliwa mashtaka ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia.

Amesisitiza mara kadha kwamba hana hatia.

Katsav alizaliwa nchini Iran na akaimbuka kuwa rais wa kwanza wa Israel aliyezaliwa katika taifa la Kiislamu.

Alichaguliwa mbunge wa chama cha Likud mwaka 1977 akiwa na miaka 30.

Mada zinazohusiana