Nyoka ajipinda katika mti wa Krismasi

Nyoka yapatikana imehipinda katika mti wa krismasi Haki miliki ya picha SNAKE CATCHER VICTORIA
Image caption Nyoka yapatikana imehipinda katika mti wa krismasi

Mwanamke mmoja amegundua nyoka yenye urefu wa mita moja aliyekuwa amejipinda katika mti wa Krismasi nchini Australia

Mwanamke huyo aliitisha usaidizi ili kuiondoa nyoka huyo katika nyumba yake huko Melbourne, Victoria siku ya Jumapili.

Mtaalam wa kushika nyoka Barry Goldsmith alisema kuwa nyoka huyo aliingia kupitia eneo la wazi katika mlango kabla ya kujipinda katika mapambo ya mti huo.

Nyoka aina ya Tiger wanaopatikana katika pwani ya Australia wana sumu kali.

Bw Goldsmith alisema kuwa mwanamke huyo alichukua hatua madhubuti baada ya kuigundua nyoka huyo.