Mkuu wa IMF apatikana na makosa

Mkuu wa IMF Christine Lagarde

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mkuu wa IMF Christine Lagarde

Mkuu wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde, amepatikana na makosa ya kutomakinika wakati alipotoa malipo makubwa ya fidia miaka 8 iliyopita, wakati akiwa waziri wa fedha wa Ufaransa.

Kesi hiyo ilisikilizwa na mahakama maalum iliyoamua kwamba haitomwadhibu wala kumpa rekodi ya uhalifu.

Lagarde alilipa pesa hizo katika mpango wa upatanishi, ambapo bwanyenye kwa jina Bernard Tapie, alipokea zaidi ya dola milioni 400.

Bodi ya IMF itafanya kikao kutathmini matokeo ya kesi hiyo, huku mawakili wa Lagarde wakisema kwamba watakata rufaa.