Ndege zinazoangusha kinyesi angani kupigwa faini India

Ndege zinazoangusha kinyesi angani kuigwa faini India
Image caption Ndege zinazoangusha kinyesi angani kuigwa faini India

Ndege nchini India zitakazoangusha kinyesi cha binaadamu kutoka angani zitapigwa faini ya Rupee 50,000 sawa na dola 736 mahakama imeamuru.

Mtu mmoja amelalama kwamba ndege zimekuwa zikiangusha uchafu huo kutoka chooni juu ya makaazi ya watu karibu na uwanja wa ndege wa Delhi.

Vyoo vya ndege huweka uchafu wa chooni katika matangi maalum.

Matangi hayo hufunguliwa na uchafu huo kumwaga ndege inapotua.

Lakini mamlaka ya anga imekiri kwamba mtiririko wa uchafu huo hutokea angani kwa bahati mbaya.

Mahakama sasa imeagiza shirika hilo la usafiri wa ndege kuhakikisha kuwa kwamba ndege haziangushi kinyesi cha binaadamu kutoka anagani wakati inapotua ama mahala popte karibu na uwanja wa ndege.