Mshukiwa wa shambulizi la Berlin auawa Italia

Polisi wa Ujerumani wametoa picha za Anis Amri

Chanzo cha picha, BKA / HANDOUT

Maelezo ya picha,

Polisi wa Ujerumani wametoa picha za Anis Amri

Mtu aliyeendesha shambulizi kwenyr soko mjini Berlin Anis Amri, ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini Milan nchini Italia.

Mtu huyo alikuwa amewafyatulia polisi risasi walipomaka awaonyeshe kitambulisho chake walipokuwa wakipiga doria eneola Sesto San Giovani. mapema siku ya Ijumaa.

Polisi mmoja aliuawa wakati wa ufyatuaji huo wa risasi,

Ujerumani imekuwa kwenye tahadhari kubwa tangu lifanyike shambulizi lililowaua watu 49.

Wakati huo huo polisi wamewakamata watu wawili katika mji wa Oberhausen baada ya kushukiwa kupanga mashambulizi.

Alama za vidole za mtu aliyeuawa vinafanana na alama za mshukiwa raia wa Tunisia ambaye aliendesha shambulizi la bomu la lori mjini Berlin siku ya Jumatatu na kuwaua watu 12.