Raia 20 wauawa kikatili mashariki mwa DR Congo

Ramani ya Kivu Kaskazini nchini DRC
Image caption Waasi wa kundi la ADF kutoka Uganda wamelaumiwa kwa mauaji ya sasa

Takriban raia 20 wameuawa katika mauaji ya kikatili katika jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kulinga na taarifa zilizotolewa na maafisa Jumapili.

Vifo hivi ni vya hivi karibuni katika wimbi la miaka miwili la ghasia katika jimbo hilo.

Mauji hayo yametokea katika mji wa Eringeti, uliopo kilomita 55 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo wa Beni, mji ambao umekuwa ukikumbwa na misururu ya mashambulio ambayo tayari yamesababisha vifo vya raia 700, kulingana na afisa katika mkoa huo Amisi Kalonda, ambaye amewalaumu waasi kutoka Uganda kwa mashambulio ya hivi karibuni.

Bwana Kalonda amesema kuwa wajumbe wa kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye idadi kubwa ya Waislam wenye itikadi kali kutoka Uganda ambao wamekuwa kwenye kanda hiyo kwa zaidi ya miongo miwili , walivamia mji huo Jumamosi mchana.

"ADF wamevamia tena wau wa Eringeti na maeneo yanayozingira mji huo asubuhi ," aliliambia shirika la habari la AFP, kutoka mji mkuu wa Kivu kusini wa Goma.

"Jana, waliwauwa raia 10. Miili mingine ya watu kumi na miwili ilipatikana Jumapili katika vijiji vinavyozingira mji ." alisema Bwana Kalonda akiongeza kuwa waathiriwa waliuliwa kwa visu au panga''

Kwa miaka miwili iliyopita eneo linalozingira mji wa Beni limekuwa likikimbwa na mauaji ya kikatili

yaliyowauwa mamia ya raia, wengi wao wakichinjwa na kunyongwa hadi kufa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Msemaji wa jeshi la Kongo Mak Hazukay amethibitisha shambulio, akisema wanajeshi ''waliwauwa waasi wa ADF " lakini akaongeza kuwa " idadi ya raia waliokufa ni kubwa".

Maafisa wa Kongo wamekuwa wakiwalaumu waasi wa ADF kwa mauaji hayo , lakini ripoti kadhaa za wataalam zimekuwa zikisema kuwa makundi mengine, yakiwemo ya wanajeshi wa serikali yalihusika katika baadhi ya mauaji.

Msemaji wa jeshi la Kongo Mak Hazukay amethibitisha shambulio, akisema wanajeshi ''waliwauwa waasi wa ADF " lakini akaongeza kuwa " idadi ya raia waliokufa ni kubwa".

Teddy Kataliki, mkuu wa shirika maarufu la kiraia katika kanda hiyo, pia alisema kuwa waliouawa ni 22.

Lakini kasisi wa kikatoliki katika eneo hilo amesema kuwa waliouawa ni watu 27 na idadi inaweza kuongezeka zaidi " kama miili ya waliouawa itabainika katika msitu" unaopakana na mji huo.

Wakati mauaji ya kikatili ya Beni yalipofanyika Oktoba 2014, ADF walijibu haraka wakishutumu makundi mauaji hayo kutekelezwa na maafisa wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na MONUSCO---Kikosi cha kulinda amani nchini DRC.

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa, mamlaka za kongo na Umoja wa Mataifa zimeshindwa kuwalinda raia na ADF limesalia kuwa ndilo kundi linalotawala, huku serikali ikisisitiza kuhusu uhusiano wa mauaji hayo na vita vya kidini vya Jihad.

Mauaji haya yanatokea huku mahusiano baina ya jamii ya kimataifa na DRC ukiwa mbaya kutokana na hatua ya rais Josep Kabila kukataa kuachia mamlaka, licha ya muhula wake kumalizika taraehe 20 Disemba.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii