Watu 11 wauawa kwenye sikukuu ya Krismas, Marekani.

Mauaji Chicago, Marekani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mauaji Chicago, Marekani

Watu 11 wameuawa katika mashambulio ya risasi kwenye mkesha na sikukuu ya Krismas mjini Chicago Marekani.

Polisi nchini humo wamesema pia kwamba watu zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyohusisha bunduki, na kuyahusisha na magenge ya uhalifu.

Idadi hiyo ya watu waliouawa imefanya jumla ya watu waliouawa kwa risasi katika kipindi cha mwaka 2016 kufikia mia saba na hamsini. Na kufanya mji huo kuongoza kwa mauaji katika kipindi cha miongo miwili.