Trump: UN ni baraza la porojo

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amelikashifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
Image caption Rais mteule wa Marekani Donald Trump amelikashifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Rais mteule wa Marekani , Donald Trump, kwa mara nyengine tena amelikashifu shirika la Umoja wa Mataifa.

Kupitia akauntI yake ya Twitter, amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi, limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na kupiga gumzo.

Hii ni baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makaazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli.

Netanyahu: Israel haitaheshimu azimio la UN

Trump: UN ni baraza la kupiga gumzo

Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina.

Azimiio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii