Aliyehamia Korea Kusini kutoka K Kaskazini asema hajuti

Thae Yong Ho
Image caption Thae Yong Ho

Mwanadiplomasia wa Korea Kaskazini ambaye alihamia nchini Korea Kusini ameiambia BBC kwamba hajuti kufanya hivyo.

Thae Yong Ho, aliyekuwa naibu wa balozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza, alisema kuwa kila mtu katika familia yake ameanza maisha mapya nchini Korea Kusini.

Amesema kuwa familia yake inafurahia uamuzi wake wa kuhamia Korea Kusini.

Serikali ya Korea Kusini ilitangaza mnamo mwezi Agosti kwamba Thae Yong Ho alikuwa amehama na familia yake kwa kutopendelea uongozi wa Korea Kaskazini chini ya uongozi wake Kim Jong Un