Marekani yapinga kuisaidia IS nchini Syria

Syria Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Waasi wa Syria na wanajeshi wa Uturuki wamekuwa wakijaribu kuchukua mji wa A-Bab kutoka IS

Marekani imetaja madai hayo kutoka kwa rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kuwa ya upuuzi

Msemaji wa serikali Mark Toner amesema madai hayo hayakuwa na msingi.

Kiongozi wa Urusi alisema kuwa ana ithibati tosha iliyoonyesha Marekani imetoa msaada kwa makundi ya Kikurdi ya YPG na PYD. Wanajeshi wa Uturuki wamekuwa wakipigana kuiondoa IS kutoka Kaskazini mwa Syria.

"Wamekuwa wakitushtumu tunaisaidia Daesh," bwana Erdogan alisema kwenye kikao cha waandishi wa habari mjini Ankara, akitumia jina mbadala la IS.

"Sasa wanayasaidia makundi ya kigaidi yakiwemo Daesh, YPG, na PYD. "Ni wazi kabisa, Tuna ithibati tosha iliyothibitishwa, pamoja na picha na hata video."

Uturuki na Marekani kushambulia ngome ya IS Syria

Syria: IS wasambaratishwa katika mji wa Dabiq

Uturuki:Kundi la IS linapaswa kutokomezwa

Erdogan aweka wazi operesheni dhidi ya IS

Wanajeshi 37 wa uturuki wameuawa katika oparesheni iliyoanzishwa mnamo Agosti kuwaondoa wanamgambo wa IS na wapiganaji wa Kikurdi kutoka eneo maalum lililoko karibu na mji wa al-Bab, ulioko kilomita 20 kutoka mpaka wa Uturuki.

Marekani imekuwa ikishirikiana na makundi ya Kikurdi nchini Syria lakini Uturuki inasema pia wanahusishwa na chama cha wafanyikazi wa Ki Kurdi, (PKK), kilichokuwa kikiendesha juhudi za mapinduzi ndani ya Uturuki kwa muda mrefu.

Aidha, muungano unaowakilisha makundi ya waasi na upinzani nchini Syria, umeyarai makundi hayo kushirikiana na juhudi zinazoendelea ili kufanikisha maafikiano ya kusitisha mapigano.

Lakini Riad Hijab, mjumbe wa kamati ya majadiliano ya amani (HNC), amesema kamati hiyo, haijaalikwa kwenye kongamano lililopendekezwa na Urusi kufanyika Kazakhstan.

Hijab amesema mikakati ya kukuza uaminifu inahitajika ili kuunda jukwaa la mazungumzo ya mabadiliko ya kisiasa anayosema yanastahili kufanyika mjini Geneva na kudhaminiwa na UN.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii