Colombia yaidhinisha sheria ya msamaha kwa waasi wa FARC

Rais wa Colombia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Colombia

Bunge nchini Colombia limeidhinisha sheria inayotoa msamaha, ambayo itawanufaisha maelfu ya waasi kutoka katika kundi la FARC.

Utungwaji wa sheria ni sehemu ya makubaliano ya amani, ambayo waasi pamoja na serikali walisaini mwezi uliopita baada ya zaidi ya miaka 50 ya vita.

Msamaha huo pia unawahusu wanajeshi wa Jeshi la Colombia.

Rais Juan Manuel Santos amesema kura ya kihistoria ilikuwa ni hatua ya kwanza katika kuimarisha amani nchini humo.

Rais Santos amekuwa ni mshindi wa tuzo ya Nobel kwa mwaka huu kutokana na juhudi zake za kufikia makubaliano.