Waasi wakubali mazungumzo ya kusitisha vita Syria

Wapiganaji wa kundi la al Sham nchini Syria
Image caption Wapiganaji wa kundi la al Sham nchini Syria

Kundi moja la waasi wa Syria limesema litakutana na maafisa wa Urusi na wale wa Uturuki kuzungumzia swala la kusitishwa kwa mapigano huko Syria.

Kundi hilo Ahrar al-Sham linasema tayari limefanya mazungumzo na Uturuki lakini bado mwafaka haujapatikana kwasababu ya kutojumuishwa kwa eneo moja muhimu lililoko karibu na Damascus kwenye mazungumzo hayo.

Hapo jana waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema nchi yake imekubaliana na Urusi na vilevile Iran kuwe na ushirikiano wa karibu katika lengo la kutafuta amani ya kudumu huko Syria.