Rais Durtete: Nilimtupa mshukiwa kutoka juu ya ndege

Rais Durtete amewaonya viongozi wafisadi nchini mwake kwamba atawatupa juu ya ndege
Image caption Rais Durtete amewaonya viongozi wafisadi nchini mwake kwamba atawatupa juu ya ndege

Rais wa Philippine, Rodrigo Duterte ametishia kuwarusha viongozi wafisadi kutoka ndege hewani akisema amefanya hivyo kitambo.

Bwana Duterte aliyasema hayo akiwahutubia waathiriwa wa kimbunga katikati ya Philippines Jumanne. Video ya hotuba yake ilichapishwa na ofisi yake.

"Kama wewe ni mfisadi, nitakubeba kutumia helikopta hadi Manila na nitakurusha nje," allisema Bwa Duterte, ambaye ameanzisha vita dhidi ya ufisadi na mihadarati.

Alitishia adhabu ya helikopta kwa yeyote atakayeiba fedha za msaada alizoahidi kutoa.

"Nimefanya hivi kitambo, kwa nini nisiweze kufanya tena?" alisema akishangiliwa na watu hao.

Haya ni madai mapya ya rais huyo ambaye amekiri kutekeleza mauaji ya kiholela. Msemaji wake amepinga madai hayo.

Mapema mwezi huu, msemaji mwingine, Martin Andanar alisema kauli za mwajiri wake zipokewa kwa makini lakini zisipewe uzito baada ya kusema kuwa aliwaua watu watatu alipokuwa Mya wa mji wa Davao nchini humo.