Jamil Makulu kutofika mahakamani bila sababu ya msingi

Uganda Haki miliki ya picha Google
Image caption Askari wa Uganda

Mahakama moja nchini Uganda imeagiza idara ya magereza kumleta mahakamani kiongozi wa kundi la uasi la- Allied Democratic Front-ADF,Jamil Mukulu ambae amekuwa mbaroni zaidi ya mwaka mmoja tangu arejeshwe nchini Uganda kutoka Tanzania akiwa anakabiliwa na mashtaka ya kuua.

Mukulu, mbali na kosa la kuua, pia alishtakiwa na makosa mengine ya uhaini na ugaidi katika mahakama hiyo pamoja na watu wengine wawili.Hata hivyo Mukulu hakufika Mahakamani licha ya kutolewa hati iliyomtaka afike mahakamani hapo jana.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Mukulu kutofika mahakamni bila kutoa sababu maalum licha ya kuwa na hati ya kumtaka afike mahakamani .

Hatua hiyo imepelekea mawakili wake kutoa malalamiko kuwa mteja wao hajatendewa haki kwa kuwa magereza haina sababu yoyote ya kushindwa kumleta mtu huyo mahakamani. kwa kuwa mteja wao ana haki kama raia mwingine yoyote yule. Hivyo ni kazi ya mahakama kuhakikisha kuwa ana hatia au laa.