Israel yawatahadharisha raia wake walioko India

India
Image caption India

Israel imewatahadharisha raia wake dhidi ya safari za kwenda India wakisema kuna hatari kubwa huenda wakashambuliwa wakiwa huko.

Wameonya hasa waepuke maeneo ya vivutio vya watalii vilivyoko kusini mashariki mwa nchi hiyo, ikiwemo maeneo ya fuo za bahari na hata vilabu vya burudani za usiku kama disco wakisema huenda kukawa na mashambulio wakati wa mkesha wa mwaka mpya.

Mwandishi wa BBC huko Jerusalem anasema Israel hutoa tahadhari kama hizo mara kwa mara lakini ni nadra kwamba wanataja maeneo maalum kama hayo.

Mada zinazohusiana