Shule ya watu waliobadili jinsia yafunguliwa India

Shule ya kimataifa ya watu waliobadili jinsia yafunguliwa nchini India Haki miliki ya picha BB Contributor
Image caption Shule ya kimataifa ya watu waliobadili jinsia yafunguliwa nchini India

Shule ya watu waliobadili jinsia imefunguliwa katika mji wa Kochi nchini India , ili kuwasaidia watu wazima walioacha shule kukamilisha masomo.

Watu waliobadili jinsia hushambuliwa nchini India na nusu yao hukosa kukamilisha masomo.

Shule ya kimataifa ya Sahaj ndio shule ya kipekee nchini India.

Itawakaribisha wanafunzi 10 walio na kati ya umri wa miaka 25 hadi 50.

Wanafunzi hao wataandaliwa kufanya mitihani ya 10 na 12 katika bodi ya mitihani ambayo hufanywa wakati mwanafunzi anapofikisha umri wa kati ya miaka 15-16 ama 17- 18 mtawalia.

Mtaala pia utashirikisha mafunzo ya kiufundi.

Mwanaharakti wa watu wanaobadili jinsia Vijayraja Mallika ambaye anasimamia shule hiyo ameambia BBC: Shule hii inalenga kuwasaidia watu waliobadili jinsia kupata kazi nzuri na kuishi katika maisha ya heshima.

''Tumesajili wanafunzi sita kufikia sasa wote wakiwa wanaume waliobadili kuwa wanawake kutoka kwa maombi 14.Kati ya viti kumi vilivyopo ,tumehifadhi kiti kimoja kwa mwanamke anayebadili jinsia kuwa mwanamume pamoja na kimoja cha mlemavu''.