Mariah Carey akatiza tamasha la kufungua mwaka

Maria Carey alikasirishwa na uandalizi huo wa tamasha
Image caption Maria Carey alikasirishwa na uandalizi huo wa tamasha

Kumekuwa na shutuma kali baada ya tamasha la nyota wa muziki Mariah Carey kufungua mwaka mpya kuathiriwa na tatizo la kimitambo

Nyota huyo wa muziki wa pop aliyekuwa akiwatumbuiza mashabiki wake katika bustani ya New York alikumbwa na matatizo ya kiufundi baada ya kulalamikia sauti mbaya na kushindwa kuimba vizuri.

Wawakilishi wake walisema kuwa waandalizi wa tamasha hilo walitaka afeli.

Lakini waandalizi hao wa Dick Clark Production walisema kuwa mpango wowote wa kumuangusha msanii yeyote ni kumuaribia jina, ujinga mkubwa na ukatili wa hali juu.

Carey alikuwa akitumbuiza moja kwa moja katika ABC kabla ya saa sita usiku na alianza vizuri lakini tatizo likaanza wakati alipokuwa akiimba kibao chake cha 1991 kwa jina Emotions.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mariah Carey na mcheza densi wake katika tamasha hiyo

Akilalamika kwamba alikuwa hasikii ,hakuweza kuimba kibao hicho na wasakataji wake wa densi walimsaidia kuendelea kutumbuiza.

Baadaye aliambia umati uliohudhuria tamasha hiyo kwamba angetaka likizo pia yeye.

''Je naweza kwenda.Najaribu kuwa mwanariadha mzuri hapa''.t

Tatizo hilo liliendelea wakati wa wimbo wake wa 2005 We belong together.

Alipunguza sauti yake lakini bado akawa anasikika katika wimbo aliorekodiwa.

''Bado sisikii vizuri'',alisema mwisho wa wimbo huo.

Carey aliambia waandalizi wa tamasha hiyo kwamba vinasa sauti vyake vilikuwa havifanyikazi mwanzo wa tamasha hilo ,mwakilishi wake alisema.