Uturuki yakaribia kumpata muuaji wa watu 39 Istanbul

Muuaji aliingia kwa nguvu kwenye ukumbi huo wa starehe na kuanza kufyatua risasi hovyo
Image caption Muuaji aliingia kwa nguvu kwenye ukumbi huo wa starehe na kuanza kufyatua risasi hovyo

Uturuki imesema inakaribia kumtambua mtu aliyefyatua risasi hovyo na kuwaua watu 39 katika sherehe za mkesha wa mwaka mpya kwenye klabu moja ya usiku mjini Istanbul.

Naibu waziri mkuu wa nchi hiyo , Numan Kurtulmus amesema wapelelezi wamekwisha gundua alama za vidole pamoja na vielelezo vingine vya mshambuliaji huyo.

Image caption Picha hii ilipigwa na CCTV ikimuhusisha mtuhumiwa huyo

Kurtulmus ameongeza kuwa Uturuki itaendelea na shughuli zake za kijeshi dhidi ya kundi la IS nchini Syria,kundi linalokiri kuhusika katika shambulizi hilo la Istanbul.