Madaktari waonya kuhusu ulaji ''keki na peremende kazini''

Madaktari wa meno wameshtumu utamaduni wa kazini wakisema ulaji wa keki na peremende unachangia matatizo ya kiafya Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Madaktari wa meno wameshtumu utamaduni wa kazini wakisema ulaji wa keki na peremende unachangia matatizo ya kiafya

Madaktari wa meno wameshtumu utamaduni wa kazini wakisema ugawanyaji wa keki na peremende unachangia matatizo ya kiafya.

Idara ya afya ya meno imesema kuwa watu wanafaa kupunguza ulaji wa keki na biskuti kazini kwa sababu vyakula hivyo vinawafanya kunenepa kupitia kiasi mbali na afya mbaya ya mdomo.

Profesa Nigel Hunt amesema kuwa wafanyikazi wanahitaji kubadilisha utamaduni wa kazini.

Ili kuweza kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari wafanyikazi wameshauriwa kutumia vyakula hivyo kama chakula cha mchana mbali na kuvificha .

Profesa Hunt ,muhadhiri wa chuo kikuu cha Royal College of surgeons ,alisema kuwa huenda wasimamizi wa afisi hizo wanataka kuwazawadi wafanyikazi, wafanyikazi kutaka kusherehekea ama mtu anayeleta zawadi afisini baada ya likizo hatua inayosababisha vyakula vya sukari nyingi kuingia afisini.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Ulaji wa vyakula vya sukari unapaswa kusitishwa,madaktari wamesema

Lakini amesema kuwa hilo linaathiri afya ya wafanyikazi na ni muhimu kufanya uamuzi wa mwaka mpya wa kukabiliana na utamaduni wa vyakula vya sukari.

''Ijapokuwa peremende hizo huenda zikawa na maana ,zinachangia unenepaji wa kupitia kiasi pamoja na afya mbaya ya mdomo,''aliongezea.

Tunahitaji kubadili utamaduni katika afisi zetu ambao unashawishi ulaji wa vyakula vya afya na unawasaidia wafanyikazi kutotumia vyakula vya sukari kama vile, keki, peremende na biskuti.