Wabunge wa upinzani wamshtaki rais Museveni ICC

Rais Museveni wa Uganda
Image caption Rais Museveni wa Uganda

Wabunge wanne wa chama cha upinzani nchini Uganda cha Forum for Democratic Change- FDC- kutoka maeneo ya magharibi mwa Uganda huko Kasese, wamemshtaki kiongozi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai -ICC, iliyoko The Hague nchini Uholanzi.

Wanasiasa hao wanamhusisha katika kile wanachokiita mauaji mabaya wakati vikosi vya usalama vilipovamia kasri la mfalme wa Rwenzururu Wesley Mumbere.

Wabunge hao chini ya kiongozi wa upinzani bungeni na mbunge wa FDC wa Kasese Winnie Kizza, wameyasema hayo leo mjini Kampala, walipokuwa wakiwahutubia waandishi wa habari.