Marekani kumsaka mtoto wa Osama Bin Laden

Osama Bin Laden alikuwa kiongozi wa Al Qaeda
Image caption Osama Bin Laden alikuwa kiongozi wa Al Qaeda

Marekani imemtaja Hamza ambaye ni mtoto wa kiume wa Osama Bin Laden katika orodha ya Magaidi.

Taarifa kutoka wizara ya ulinzi zinasema Hamza Bin Laden akiwa katika umri wa miaka ishirini amekuwa kiongozi makini wa kundi la Al Qaeda ambao ni wapiganaji wa kundi lililoanzishwa na baba yake.

Taarifa zinasema amekuwa makini katika suala hilo kwa kufuata nyayo za baba yake kwa kujiunga na jihadi na kusambaza ujumbe wa sauti kwa niaba ya kundi la Al Qaeda na kuchochea mashambulizi dhidi ya nchi za Magharibi.

Kwa sasa Atazuiliwa kufanya biashara na wananchi wa Marekani na mali zake zitataifishwa.

Kiongozi mkuu wa usalama wa kundi la Al Qaeda Ibrahim al-Banna ametajwa katika orodha hiyo pia.

Marekani itatoa ofa ya dola Million tano kwa atakayesadia kukamatwa kwa al-Banna.