Kwa Picha: Afrika 30 Desemba 2016 - 6 Januari 2017

Mkusanyiko wa picha bora zaidi kutoka Afrika wiki hii:

Nigeria Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkesha wa Mwaka Mpya, wachekeshaji wanatumbuiza jukwaani katika tamasha la One Lagos fiesta mjini Lagos, Nigeria
Lagos Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanamuziki na wasakata ngoma pia walitumbuiza usiku huo kwenye tamasha hilo Lagos
Mwanga waangaza kwenye piramidi (maharam) viungani mwa mji wa Cairo, Misri kuukaribisha Mwaka Mpya Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanga waangaza kwenye piramidi (maharam) viungani mwa mji wa Cairo, Misri kuukaribisha Mwaka Mpya
Rades. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashabiki wa klabu ya Club Africain ya Tunisia wakipeperusha bendera wakati wa mechi ya kirafiki na Paris Saint-Germain mjini Rades Jumatano
A disguised and painted man does a tongue trick during a street parade in Cape Town on 2 January Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mshiriki katika maonyesho katika barabara ya mji wa Cape Town Jumatatu tarehe 2 Januari
... huku mtu mwingine aliyevalia kwa njia ya ucheshi katika tamasha la kitamaduni Winneba, Ghana Haki miliki ya picha AFP
Image caption ... huku mtu mwingine aliyevalia kwa njia ya ucheshi kama tumbili katika tamasha la kitamaduni Winneba, Ghana
Uhuru Park, Nairobi, Kenya Haki miliki ya picha AP
Image caption Hapa mtoto Mkenya anaonekana akicheza kwenye eneo la kutelezea katika bustani moja mjini Nairobi siku ya Mwaka Mpya
Sadio Mane Haki miliki ya picha AFP
Image caption Winga wa Senegal Sadio Mane akishiriki mazoezi JUmatano mjini Dakar timu ya taifa lake ikijiandaa kwa fainali za Kombe la Taifa Bingwa Afrika baadaye mwezi huu
Yei Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Na hapa, raia wa Sudan Kusini wanaonekana wakinunua mboga katika soko la Yei, kusini magharibi mwa mji mkuu Juba siku ya Mwaka Mpya
Ceuta Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumanne, mhamiaji wa miaka 19 kutoka Gabon aligunduliwa amefichwa kwenye mkoba akisafirishwa kutoka Morocco hadi eneo linalomilikiwa na Uhispania la Ceuta
Helderberg Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ndege inaonekana ikimwaga maji kujaribu kuzima moto katika milima ya Helderberg karibu na Cape Town nchini Afrika Kusini siku ya Jumatano
Cape Town Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hapa, wazima moto wanaonekana wakijaribu kukabiria na moto huo karibu na mji wa Cape Town

Picha kwa hisani ya AFP, EPA, Reuters

Mada zinazohusiana