Mahakama Marekani yamhukumu kifo mzungu mbaguzi kwa mauaji

Dylann Roof Haki miliki ya picha AP
Image caption Dylann Roof

Mahakama nchini Marekani imemuhukumu adhabu ya kifo mzungu mwenye msimamo mkali, ambaye aliwaua waumini tisa weusi katika kanisa moja, Carolina ya Kusini.

Dylann Roof alikutwa na hatia mwezi uliopita kwa zaidi ya mashtaka 30, ikiwemo uhalifu wa chuki.

Katika maelezo yake ya mwisho kwa mahakama hakuonesha kujutia makosa yake na kusema bado anahisi alipaswa kufanya mauaji hayo.

Mwezi Juni 2015, alikwenda katika kanisa moja la watu wenyea asili ya Afrika mjini Charleston na kufyatua risasi wakati somo la dini likiendelea.

Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa kuhusiana na masuala ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani na kumlazimu Rais Barack Obama kutaka kumalizwa kwa ghasia zinazosababishwa na matumizi ya bunduki.